Latest Post

LOWASA AKIMBIZA WANACHAMA WA CHADEMA LUDEWA ,WAHAMIA ACT WAZALENDO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, August 21, 2015 | 4:20 PM


Add caption
Wanachama  wa Chadema wilaya ya  Ludewa  mkoa wa  Njombe  wakiandamana  kupinga  maamuzi ya  chama  hicho  kukata  jina la mshindi  wa  kura  za maoni na  kumteua  aliyeshindwa ,mbali ya  kuandamana  pia  wanachama  hao  zaidi ya  500  walikihama  chama  hicho na  kujiunga na  ACT  Wazalendo
Wanachama  wa  Chadema  waliohamia ACT wazalendo  wakiwa na  mabango ya  kukituhumu  chama   hicho  kwa  kukiuka  Demokrasia


kadi na nyalaka  za Chadema  zikichomwa moto
Wanachadema  wakiwa  nje ya  ofisi ya  ACT  Wazalendo  ambako  walifika  kuomba  kujiunga huko
kadi  za  chadema  zikiteketezwa  kwa  moto


wana chadema  wakiwa na mabango
Hasira  za  kukatwa  kwa  mshindi  wa kura  za maoni Ludewa


wanachadema  wakijiandaa kwa maaandamano ya amani  kujiengua na  Chadema  na  kujiunga  ACT  wazalendo
Bango  likimtaka  aliyeteuliwa na chama  kwenda  kugombea  jimbo la Hai kwa Mbowe


Add caption
Mwanzo  wa maandamano ya  kujiengua na  Chadema
Add caption
wana Chadema katika maandamano  ya  kupinga  uonevu ndani ya  chama
Tuhuma  dhidi ya  Chadema Taifa


Wanachadema  katika maandamano ya  kupinga mshindi  kutemwa


Wanachadema  waliojiengua na  kujiunga na ACT  wazalendo  wakiwa nje ya ofisi ya  Chadema  wilaya ya  Ludewa
barua  ya  tuhuma  za  mteuliwa  kutoa  ahadi ya  rushwa hii hapa

barua  ikionyeshwa  kwa  wanahabari na  wanachadema
Ni  full jaziba  kwa  wana Chadema  Ludewa
Wanachadema  wakiwa  nje ya  ofisi   ya chama  wilaya  walikokwenda  kurudisha  kadi kabla ya  kuhamia ACT wazalendo
Aliyekuwa mwenyekiti wa BAWACHA  wilaya ya  Ludewa akionyesha  kadi ya  ACT  wazalendo
Aliyeenguliwa Bw  Haule  akiwapongeza wana Chadema kwa kuhamia pamoja  ACT  wazalendo
Wanachadema  wakirudisha  kadi  za chamna  hicho na kujiunga na ACT  wazalendo
Baadhi ya  nguo  na kadi  zikiandaliwa  kuchomwa  moto
katibu wa ACT  wazalendo  Ludewa Alfred Ulaya  akionyesha kadi  za  Chadema 
Wanachadema  wakijipata  kuhamia  ACT wazalendo
Kadi  zikiwa  zimekusanywa kwa kuchomwa  moto
mwana  Chadema  akichoma  moto kadi  za  Chadema Ludewa  kupinga  uonevu  ndani ya  chama  hicho
Add caption
Hivi  ndivyo kadi  zinavyoteketezwa  kwa  moto  baada ya  wana Chadema  kujiengua na  chama  hicho na kujiunga na ACT  wazalendo 


Mabango  ya  kuagana na Chadema  kwa  wana Ludewa


Bango  likionyesha  Chadema kura  za Chadema  Urais X ,Ubunge X na udiwani X huku  likimaliza kwa  kusema  msituchagulie
Mwanachama wa Chadema  akiongea  kwa jazba  juu ya hali ya mambo ndani ya  Chadema kabla ya  kujiunga na ACT  wazalendo
Ofisi ya  Chadema  wilaya  ikiwa  imefungwa  wakati  wanachadema  walipofika  kurudisha  kadi zao


Kadi  ya  ACT  baada ya  kuhama  Chadema
Makada  wapya  wa ACT  kutoka  Chadema 


Aliyekuwa mshindi wa kura za maoni  akionyesha  barua  nyenye  siri nzito  za  mteuliwa  kununua nafasi hiyo
Bw Haule  akijiandaa  kuchoma moto vifaa vyake vya Chadema kabla ya  kujiunga na ACT wazalendo
........................................................................................................   

-->
*Wafanya Maandamano Makubwa. Wachoma Moto Kadi
* Ofisi  ya Chadema Wilaya  Nusuru  Ichomwe Moto;  Viongozi  wakimbia; Watelekeza ofisi
 Na MatukiodaimaBlog,Ludewa
WANACHAMA zaidi  ya 500 wa  Chama  Cha  Demokrasia  na Maendeleo ( Chadema)  Wilayani Ludewa  Mkoani  Njombe wamekihama  chama  hicho  na kujiunga na  chama  cha  ACT Wazalendo   wakipinga  hatua ya  uongozi  wa  juu  wa  chama  hicho kukata  jina  la  mshindi  wa  kwanza wa  kura  za maoni Bw. Ocol Haule  na kumteua aliyekuwa mshindi  wa  pili katika mchakato huo Bw Bartholomeo Mkinga .

Wanachama  hao ambao  kutoka  kata  mbali mbali  za  wilaya  ya  Ludewa wamefanya maandamano hayo ya amani leo  kuelekea   ofisi ya  Chadema  wilaya  huku wakitishia    kuichoma moto  ofisi  hiyo  baada ya  viongozi  wake  kuifunga,  kuitelekeza  na kukimbia kunusuru maisha yao. 

Wakizungumzia  hatua   hiyo ya kupinga  maamuzi ya  chama ngazi ya  taifa wanachama hao Bi Hongera  Gama,  Taukile Mapunda  na aliyekuwa  Mwenyekiti  wa Baraza la  Wanawake  (BAWACHA) wilaya ya Ludewa Bi. Sophia Mtega  walisema  kuwa wanachama  walikuwa na  imani  kubwa na mshindi  wa kura  za maoni  kwani alifanya kazi kubwa ya kukijenga chama na sio  huyo  waliomuacha katika  kura  za maoni .

“Kinachoendelea sasa hivi ndani ya CHADEMA ni ufisadi mtupu,” alisema Bi. Gama akiongeza kuwa yeye binafsi alitoka  CCM na  kujiunga na Chadema  kutokana na  mapungufu  yaliyokuwepo   ndani ya  CCM  ila  kinachoendelea  kwa  sasa  ndani  ya  Chadema  anajuta kuingia Chadema  na  hivyo  ameamua  kuhama chama  hicho  kumfuata mtu  wao  waliyemchagua popote atakakokwenda .

“ Mwenendo  wa  chadema  kwa  sasa ni  wa  ovyo  zaidi  kuliko  chama  chochote  cha siasa hapa nchini tulikuwa  tukishuhudia  CCM  watu  wakikatwa ila  leo  ndani  ya Chadema  imekuwa  ni kawaida  kuona  wale  waliochaguliwa na  wanachama kukatwa na   watu  wachache akiwemo  mwenyekiti  wa Taifa  wa  chama  hicho Freeman Mbowe …..tumechoka tunahitaji kwenda  kupata Demokrasia ya  kweli ACT wazalendo sio  ndani ya  chadema”

Huku Bw Mapunda akidai  kuwa siasa  za  ukabila  zinaendelea  kukitesa  Chadema  na  kuwa  suala   hilo  la ukabila  na  kuwakumbatia  mafisadi  ndilo  ambalo  linaendelea  kukitafuna chama hicho pia  siasa za  ukanda na  kukumbatia  ufisadi  imekuwa ni kawaida  Chadema.

Hivyo alisema  katika kuhakikisha  wana  Chadema  wilaya ya  Ludewa na   kote  nchini  wanapinga siasa  za  ukanda na zile za kuwachukua  watu  wenye  tuhuma  za  ufisadi kugombea  ndani ya  chama  hicho  ni lazima  wanachadema  kuungana  kupinga hali  hiyo  kwa  kuhama  ndani  ya  chama  hicho na  kujiunga na ACT  wazalendo.

Aliyekuwa  mwenyekiti wa BAWACHA  wilaya ya  Ludewa Bi Mtenga  alisema  kuwa  uonevu  na  rushwa  vimechangia  wanachama na  wananchi kukosa  imani kabisa na  chama  hicho na  sasa badala ya  kuwa chama cha  wanyonge  kimekuwa ni chama  cha  wenye  pesa na mafisadi jambo ambalo  wao kama  wananchi wa chini hawapo  tayari  tena  kukaa ndani ya  Chadema.

Akimkaribisha  mgombea ubunge   huyo  aliyekatwa ndani  ya  Chadema  Bw Haule na  wanachama  zaidi ya 500 wa  chadema , katibu  wa  ACT wazalendo  wilaya ya  Ludewa Bw Alfred Ulaya  alisema  kuwa  pia  alipata  kuwa  kiongozi  ndani ya  Chadema  wilaya  ya  Ludewa  ila alihama  pamoja na  viongozi  wengine  kutokana na siasa  za chuki ndani ya chama  hicho na hatua ya  kukumbatia  ufisadi.

Hivyo  alisema  wanachama  hao  hawajachelewa  kujiengua na chadema na kujiunga na chama cha  ACT  wazalendo kwani ni chama chenye  misingi  bora na chama pekee  chenye malengo sahihi ya kulikomboa  Taifa  na Chadema na  pamoja na umoja  wao  wa vyama  vinavyo unda katiba ya  wananchi (UKAWA) ni CCM B  hivyo  lazima watanzania  wapenda mabadiliko lazima  kuchagua ACT wazalendo.

Katibu  huyo  alisema  kwa  wanachama  wote  ambao  wamejiengua na Chadema na kujiunga na ACT wazalendo wakiwemo makatibu na  wenyeviti wa kata   zaidi ya 10  waliojiunga na ACT wazalendo na viongozi  wengine  watakuwemo ndani ya  chama  hicho na vyeo  vyao kama  walivyotoka  Chadema.

Kwa upande  wake mgombea  huyo aliyeenguliwa  kugombea  ubunge  mbali ya  kushinda kura za maoni Bw Haule  alisema  kuwa kimsingi aliyeteuliwa  kugombea nafasi hiyo alikuwa amewaandikia barua baadhi ya  viongozi ngazi ya  wilaya  ya  kuwaahidi kuwapa  pesa ,kufungua  duka la  vifaa  mbali mbali pamoja na kuwahonga  pikipiki barua  ambayo aliinasa na  kuwaonyesha  wanachama  hao.

Pia  alisema kimsingi baada ya  kuenguliwa  kugombea nafasi hiyo  alitaka  kukaa kimya kama  aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema Dr  Slaa ila  akaona  kukaa kimya  bado  si jibu na  hivyo kuamua  kujiunga na ACT wazalendo na  kuweka  uozo  huo  wazi.

Bw  Haule  alisema  kuwa kwa  sasa atahakikisha anazunguka jimbo nzima  kufikisha  kilio  chake kwa  wana Chadema  na  kupinga kwa nguvu  zote wagombea wa udiwani na ubunge wa Chadema kupewa kura na  kuwa kwa  sasa uhai  wa Chadema katika  wilaya  hiyo umekufa  rasmi .
 BANDA LA ASAS DAIRIES LTD LAVUTIA WENGI MAONYESHO YA SABA SABA DAR ES SALAAM

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, July 6, 2015 | 2:48 AM

Rais Dr Jakaya Kikwete akipata  maelezo ya  bidhaa  za Asas Daireis Ltd  kutoka kwa afisa masoko  wa kampuni  hiyo  Bw Jimy  alipotembelea  mabanda mbali mbali  katika  maonyesho ya  sikukuu ya   sabasaba yanayotaraji  kuhitimishwa kesho jijini Dar es salaam
Rais  Dr  Kikwete  akipata  maelezo ya  bidhaa za Asas Daireis Ltd kampuni  hii  ni  ndio kampuni bora ya  usindikaji maziwa nchini Tanzania kwa miaka mitatu  mfululizo sasa
Rais  Dr  Kikwete  akitazama  baadhi ya  bidhaa zenye ubora  za kampuni ya Asas Daireis Ltd
Rais  Dr  Kikwete  akifurahia  baada ya  kutembelea  banda ya Asas DaireisLtd jijini Dar es Salaam
Wananchi mbali mbali  wakitembelea  banda  ya Maziwa ya  Asas katika  viwanja  wa Sabasaba jijini Dar es Salaam
Na MatukiodaimaBlog
BANDA la  kampuni ya maziwa ya  Asas Dairies Ltd ya  mkoani Iringa lililopo  limeendelea  kuwavuta  wananchi   na  viongozi mbali mbali  wanaotembelea  viwanja  wa  Saba saba jijini Dar e Salaam  kulitembelea  kupata  bidhaa  zake 
Banda   hilo  ambalo  wiki  iliyopita  lilitembelewa na Rais Dr  Jakaya  Kikwete na  viongozio  mbali mbali  limeendelea  kuvutia  wananchi  wengi  wanaotembelea maonyesho  hayo  kupenda  kufika  kupata  bidhaa mbali mbali  .
Baadhi ya  wananchi  waliofika katika  banda   hilo  walisema  kuwa  wamevutiwa  zaidi ya  bidhaa  zenye  ubora  zinazotengenezwa na kampuni hiyo ya  Asas Dairies  Ltd kutoka mkoani  Iringa na   hivyo kulazimika  kumiminika  zaidi  kupata  bidhaa pamoja na kupata  elimu mbali mbali ya  ubora  wa  bidhaa  hizo .
Alisema Amina  Athuman  ambae ni mmoja wa  wateja  waliofika katika banda   hilo kupata  bidhaa  mbali mbali , kuwa yapo makampuni  mengi ya maziwa ila ubora  wa bidhaa  za maziwa  zinazotengenezwa na kampuni  hiyo ya Asas Dairies Ltd  ndizo  ambazo  zinawavutia  watu wengi  zaidi  kufika katika banda  hilo.
" Mimi  nilikuwa nasikia tu juu ya ubora  wa maziwa  haya toka mkoani Iringa ila baada ya  kufika hapa  nimeshuhudia na  kuanzia  leo  sihitaji maziwa na  bidhaa nyingine kama  hizi  nje ya Asas Dairies Ltd " 
Huku John Mwene  akieleza  kufurahishwa  zaidi na hatua  ya  Rais wa nchi Dr  Kikwete  kutembelea  mabanda  ya  wakulima mbali mbali  likiwemo  banda  hilo la Asas kwani ni ukweli  usiopingika kuwa kwa  Tanzania kampuni  hiyo ya  Asas Dairies  Ltd imeonyesha  uwezo  mkubwa wa kuzifanya bidhaa zake  kuendelea  kuwa na ubora  kwa miaka  mitatu mfululizo.
Kwani  alisema kampuni  kuongoza  miaka mitatu  mfululizo ni jambo la  kujipongeza na kuwa  si rahisi  kwa kampuni kushikilia ubora  wake kwa miaka miwili mfulilizo ila kampuni hiyo imeweza kufanya  hivyo .
Alisema ni jambo la nchi kupitia bodi ya maziwa  na wizara   husika kuangalia  kutoa uwezeshaji  zaidi kwa makampuni bora  ili  kuwezesha  bidhaa zake  kuingizwa katika  soko la dunia . 
Afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy Kiwelu pamoja na kumpongeza Rais Dr Kikwete kwa  kutembelea  banda  lao na kupongeza kwa ushiriki na ubora  wa bidhaa  zao bado  aliwashukuru  wananchi  wanaoendelea  kutembelea banda  hilo .
Alisema kuwa mbali ya kampuni  hiyo kuonyesha  ushiriki mzuri katika maonyesho  hayo ya saba saba bado  wamekuwa  wakishiriki maonyesho mbali mbali yakiwemo yale ya nane nane kwa kushiriki katika kanda mbali mbali na  kuwataka  wananchi wa kanda  zote  nchini kujipanga kwa ajili ya kutembelea mabanda yao wakati wa nane nane mwaka  huu .
Kuhusu kuendelea  kuongoza kwa  ubora  alisema  kuwa hivi  sasa ni  mwaka  wa tatu mfululizo bado  bidhaa  zao  nyingine  zimeendelea  kushinda medali mbali mbali na kuonyesha uwezo mkubwa wa kampuni  hiyo katika ubora .

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA